Unguja. Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba limewakamata watuhumiwa zaidi ya 20 kwa tuhuma mbalimbali kufuatia msako na doria zilizofanyika kisiwani humo.
Miongoni mwa waliokamatwa katika msako huo ulioanza Septemba 23, hadi leo Oktoba 21,2026 ni pamoja na watuhumiwa tisa wanaohusishwa na tukio la mauaji ya mwanafunzi Raiyan Hemed Amour (15).
Katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo na Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, upelelezi unaendelea na utakapokamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria kujibu tuhuma zinazowakabili.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanada wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, William Mwampaghale mwanafunzi huyo lilitokea Oktoba 2, 2026. Taarifa hiyo imeeleza kuwa Oktoba 2, 2026 mwanafunzi Raiyan Hemed Amour aliripotiwa kupotea.
Siku mbili baadaye, Oktoba 4, 2026 saa 3:20 asubuhi, mwili wa Raiyan ulipatikana katika kichaka huko kijiji cha Kwale Mpona, Shehia ya Finya, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba. Ukiwa umekatwa kiganja cha mkono wa kulia kwa kutumia kitu chenye ncha kali.
(Imeandikwa na Jesse Mikofu)

