

Mavunde ataka Stamico ishindane na mashirika makubwa
Dodoma. Waziri wa Madini, Anthony Mavunde ameligiza Shiriki la Madini la Taifa (Stamico) kuwa mshindani mkubwa miongoni mwa mashirika barani Afrika kwani inawezekana.
Mavunde amesema rasilimali walizonazo Stamico ikiwemo leseni za umiliki wa migodi mikubwa hawapaswi kuwa ni watu wa kulialia zaidi ya kuwa mfano kwa wengine.
Waziri ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Novemba 7, 2026 kwenye hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha nishati safi na salama ya Rafiki Briquettes, kilichojengwa Chigongwe jijini Dodoma.
Hata hivyo, amepongeza mabadiliko yaliyofanyika ya hivi karibuni kutoka shirika lililokuwa kwenye orodha ya kufutwa lakini limefika hatua ya kuzalisha mabilioni ya fedha.
Kwa mujibu wa Mavunde, miaka michache shirika lilikuwa likiingiza mapato ya Sh1 bilioni na likawekwa kwenye orodha ya kufutwa lakini kwa sasa wanaingiza Sh89 bilioni na wameanza kujitegemea kwa kila kitu lakini akasema wanaweza kupata mapato zaidi.
“Ndoto yangu ni kuwaona mnakuwa Shrika kiongozi barani Afrika, hapa nchi muwaze kushindana na Geits Gold Mine, Ashanti na Barrick, fursa kubwa tumewapa ni kazi kwenu kuitumia,” amesema Mavunde.
Kwa mujibu wa Waziri, Serikali imewapa Stamico leseni za migodi muhimu ya Nachingwea na hivyo karibuni wamewapa leseni ya kuchimba kwenye madini muhimu ya kutengeneza vifaa vya simu vipuri vya ndege katika moja ya maeneo Morogoro.
Amewataka kuanza uzalishaji wa umeme katika mgodi wao wa Kiwila lakini wamesisitiza wafanye kazi kwa kushirikiana na wengine.
Mkurugenzi Mkuu wa Stamico, Venance Mwase amesema matumizi ya nishati safi yaliwafanya wabuni viwanda vya kutengeneza Mkuu ambako leo wamezindua kiwanda cha nne kwenye malengo.
Mwase amesema katika siku za hivi karibuni Watanzania wengi watafikiwa kwani muda wowote watazindua viwanda kama hivyo katika miji ya Geita na Tanga.
Mkurugenzi ametaja Taasisi za Umma wa kuwa wateja wao wakubwa ikiwemo magereza na shule za Umma.
Ametaja thamani ya kiwanda kilichozinduliwa ni Sh3.7 bilioni na kina uwezo wa kutengeneza tani 20 za mkaa kwa saa moja.
Ametaja miongoni mwa mambo yaliyokwenda sambamba na uzinduzi ni ugawaji wa makontena kwa mawakala, uzinduzi wa magari na pikipiki na leseni za utambuzi kwa watoa huduma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Stamico, Balozi Simon Siro amezungumzia changamoto wanazokutana nazo ni baadhi ya Taasisi kubwa kutokulipa madeni yao, jambo linaloweza kuwarudisha nyuma kwenye juhudi zao.




Leave a Reply