

Jeshi la Polisi laonya wanaohamasisha kufanyika vurugu
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi nchini, limewaonya baadhi ya viongozi wa dini, wanaharakati na wanasiasa ambao wamekuwa wakifanya vikao vya siri vya kuhamasiha watu kutaka kujiingiza kwenye uhalifu.
Katika tamko lake kwa umma alilolitoa leo Jumatatu Oktoba 26,2026, Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime amesema, kumekuwepo na mipango, matamko na uhamasihaji unaofanywa na viongozi hao kisirisiri kupitia vikao vya ndani.
Katika vikao hivyo amesema kumekuwepo na uhamasishaji wa wazi wenye nia au mwelekeo wakutaka kuhamasisha watu kutaka kujiingiza kwenye vitendo vya vya uhalifu.
“Vitendo hivyo vya kihalifu vinavyopangwa ni pamoja na kufanya vurugu au fujo,kuharibu miundombinu inayotumiwa kutoa huduma kwa umma, mali za umma na binafsi.
“Jeshi la Polisi Tanzania linawahakikishia kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama na kwa kutumia taarifa zinzoendelea kupokea linafuatilia kwa karibu ikiwa ni pamoja na kuwakamata wahusika wa mipango hiyo kwa hatua zaidi za kisheria,”ameeleza Misime kwenye taarifa hiyo.
Aidha ametoa onyo kwa wanaojihusisha kwa namna moja au nyigine katika vitendo hivyo vya uhalifu vyenye mwelekeo wa kufanya fujo na kuharibu mali, kuacha kwani jeshi hilo halitasita kuchukua hatua kali kwa mujibu wa sheria kwa yotote ataatakayebainika kujihusisha na mipango hiyo ya kihalifu .
Kwa upande wa wananchi, jeshi hilo limetoa wito kwa kuendelea kuzingatia sheria za nchi na utii wa sheria bila shuruti kwa kuwa ndio msingi wa aman, utulivu na usalama wa Taifa.
“Jeshi la Polisi Tanzania linaenedelea kutekeleza majukumu yake ikiwemo kulinda amani, utulivu na usalama,”amesema Misime .
You may also like


Mangapwani kuwa kitovu cha mapato ya forodha


Leave a Reply